Saturday, March 12, 2016

FULL TIME: NORWICH CITY 0 v 0 MANCHESTER CITY, SARE YAWADUWAZA MASHABIKI!


Manchester City Jana walikwaa mkenge katika nia yao ya kutwaa Ubingwa baada ya kubanwa kwa Sare ya 0-0 huko Carrow Road na Norwich City wakaty Bournemouth ikishinda Nyumbani 3-2 walipoifunga Swansea City huku Stoke City wakipigwa kwao 2-1 na Southampton.
Matokeo hayo yamewaacha City wakiwa Pointi 9 nyuma ya Vinara Leicester City huku Mechi zikibaki 9.
Southampton walipata ushindi wa 2-1 kwa Bao za Graziano Pelle na Saido Mane waliofunga Dakika za 11 na 30 na Stoke kupata Bao lao pekee Dakika ya 52 Mfungaji akiwa Arnautovic.
Mane alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 91 baada ya Kadi za Njano mbeli.

Huko Carrow Road, Bao za Gradel. Dakika ya 37, King, 50 na Cook,78, ziliwapa Wenyeji Bournemouth ushindi wa 3-2 dhidi ya Swansea waliofunga Bao zao kupitia Barrow, 39, na Sigurdsson, 62.
Huo ni ushindi wa 3 mfululizo kwa Bournemouth kwenye Ligi.