Thursday, March 10, 2016

GENNARO GATTUSO ALILIA KAZI YA OLD TRAFFORD, ASEMA YU TAYARI KUTOKA ITALY KWA MGUU HADI ENGLAND ILI APATE KAZI HIYO!

MCHEZAJI wa zamani wa AC Milan na Timu ya Taifa ya Italy Gennaro Gattuso yuko tayari kutembea kwa mguu kutoka Italy kwenda Manchester ikiwa atapata kazi ya kuiongoza Manchester United.
Gattuso, mwenye Miaka 38, alitwaa Kombe la Dunia Mwaka 2006 akiwa na Italy na kubeba UEFA CHAMPIONS LIGI mara 2 akiwa na AC Milan chini ya Carlo Ancelotti.
Lejendari huyo amesema Siku zote anahusudu Soka la England na ari ya Wachezaji na Mashabiki wake ikithibitisha mapenzi yao.
Akiongea na Gazeti la England The Sun, Gattuso alihojiwa ikuwa yuko tayari kumrithi Meneja wa Man United Louis van Gaal na yeye akajibu: "Nitatembea kwa mguu kwenda huko. Nitaenda hata kesho. Siku zote Sir Alex Ferguson ameniheshimu na daima naihusudu Ligi ya England ambayo kwangu ndio Ligi bora Duniani!"
Aliongeza: "Hapa Italy sie ni mafundi wa mbinu lakini England unaona Wachezaji wenye kasi na nguvu kubwa miguuni!"
Hivi sasa Gattuso ni Meneja wa Klabu ya Serie C, Pisa, na pia aliwahi kuwa Meneja huko Sion, Palermo na OFI Crete.