Wednesday, March 23, 2016

JOSE MOURINHO NA PEP GUARDIOLA KUKUTANA USO KWA USO HUKO CHINA


Pep Guardiola atapambana na Mahasimu wao wakubwa Manchester United katika Mechi zake za kwanza Klabuni hapo katika wadhifa wake mpya.
Klabu hizi za Manchester zitakutana huko Bird's Nest Stadium huko Beijing, China, Jumatatu Julai 25 ikiwa ni moja ya Mechi za Kirafiki kwa ajili ya kujitayarisha na Msimu mpya ambapo Timu kubwa Duniani hujumuishwa kwenye Mashindano ya kugombea International Champions Cup.

Mwishoni mwa Msimu huu, Guardiola atambadili Bosi wa sasa City Manuel Pellegrini.