Thursday, March 17, 2016

KLABU BINGWA ULAYA DROO KUFANYIKA KESHO IJUMAA

Klabu 8 toka Nchi 5 Kesho Ijumaa zitatumbukizwa kwenye Chungu kimoja kwenye Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, kwenye shughuli itakayofanyika huko Nyon, Uswisi.
Droo hii iko wazi ikimaanisha Timu za Nchi moja zinaweza kukutanishwa na hivyo upo uwezekano wa, mathalani, Real Madrid na Barcelona kukutana.

Klabu zilizofuzu kuingia Robo Fainali:
-Atlético Madrid
-Bayern M√ľnchen
-Barcelona
-Benfica
-Manchester City
-Paris Saint-Germain
-Real Madrid
-Wolfsburg


Mechi za Robo Fainali zitachezwa Tarehe Aprili 5 na 6 na Marudiano ni Aprili 12 na 13.