Friday, March 4, 2016

LA LIGA: BARCA WAWEKA REKODI WAKIICHARAZA 5 -1, VALLECANO WAKIUMALIZA 9 UWANJANI, MESSI APIGA HAT-TRICK!

WAKIWA Ugenini huko Estadio Teresa Rivero, Mabingwa na Vinara wa La Liga, Barcelona, wameicharaza Rayo Vallecano Bao 5-1 na kuweka Rekodi mpya huko Spain ya kutofungwa katika Mechi 35.
Barca walitangulia kufunga Bao 2 katika Dakika za 22 na 23 kupitia Ivan Rakitic na Lionel Messi na kisha Vallecano kubaki Mtu 10 katika Dakika ya 42 kufuatia Kadi Nyekundu kwa Diego Llorente.
Messi allipa Bao la 3 Barca Dakika ya 53 na Manucho, Mchezaji wa zamani wa Man United, kuipa Vallecano Bao lao pekee lakini Dakika ya 67 wakabaki Mtu 9 baada ya Manuel Iturra kupewa Kadi Nyekundu na kutolewa Penati ambayo Luis Suarez alipiga na kuokolewa.
Barca waliongeza tena Bao 2 Dakika za 72 na 86 kupitia Messi na Arda Turan na kuibuka kidedea 5-1 na kuongoza La Liga wakiwa Pointi 8 mbele ya Atletico Madrid na Pointi 12 mbele ya Real Madrid.
Pia ushindi huu umewafikiza Mechi 35 bila kufungwa na kuibomoa Rekodi ya Real ya kutofungwa Mechi 34 waliyoweka Msimu wa 1988/89.