Sunday, March 6, 2016

LA LIGA: EIBAR 0 v 4 FC BARCELONA, MESSI AIPAISHA KILELENI BARCA AKIFUNGA BAO MBILI LEO!


Wakicheza Ugenini huko Ipurua Municipal Stadium, Mabingwa Watetezi na Vinara wa La Liga Barcelona Leo wameiwasha SD Eibar Bao 4-0 na kupaa kileleni wakiwa Pointi 11 mbele ya Atletico Madrid ambao wanacheza baadae Leo.
Bao za Barcelona hii Leo zilifungwa na Munir El-Haddadi, Dakika ya 8, Lionel Messi, Dakika ya 41 na Penati ya Dakika ya 76 huku Luis Suarez akipiga Bao la 4 Dakika ya 84.