Monday, March 21, 2016

LA LIGA: RONALDO, BENZEMA, BALE WAIFANYIA KITU MBAYA SEVILLA CHA BAO 4-0, SASA WAELEKEZA NGUVU ZAO NOU CAMP!

Benzema akipongezwa baada ya kutuma salaam ya baoCristiano Ronaldo alikosa Penati lakini alimudu baadae kupachika Bao wakati Real Madrid inaichapa Sevilla 4-0 Uwanjani Santiago Bernabéu hapo Jana.
Ushindi huo umeifanya Real, ambayo ipo Nafasi ya 3, ikate pengo lao na Timu ya Pili Atletico Madrid kuwa Pointi 1 tu huku Barca wakiwa kileleni Pointi 9 mbele ya Atletico.

Mechi inayofuata kwa Real ni ile El Clasico huko Nou Camp hapo Aprili 2. 

Bao nyingine za Real zilifungwa na Karim Benzema, Gareth Bale na Rodriguez Jese. Mbali ya Ronaldo kukosa Penati, hata Sevilla nao walikosa Penati iliyopigwa na Kévin Gameiro.
Huko Estadio El Madrigal, Mabingwa wa Spain na Vinara wa La Liga, FC Barcelona, wameumwaga uongozi wa 2-0 wa Kipindi cha Kwanza na kulazimishwa Sare ya 2-2 walipocheza Ugenini na Villareal.

Barca walitangulia kufunga Bao 2 katika Dakika za 20 na 41 Wafungaji wakiwa Ivan Rakitic na Penati ya Neymar.
Villareal walizinduka na kufunga Dakika za 57 na 63 kupitia Cedric Bakambu na Jeremy Mathieu aliejifunga mwenyewe.
Jana, Atletico Madrid, ambao wako Nafasi ya Pili nyuma ya Barca, walifungwa 2-1 wakicheza Ugenini na Sporting Gijon licha ya kuongoza kwa Bao la Dakika ya 29 la Antoine Griezmann baada Gijon kuibula Kipindi cha Pili na kupiga Bao 2 kupitia Antonio Sanabria, Dakika ya 79, na lile la ushindi la Dakika ya 89 la Carlos Castro.