Saturday, March 12, 2016

FULL TIME: BARCELONA 6 v 0 GETAFE, MESSI NA NEYMAR WAISOGEZA BARCA KILELENI TENA!


Mabingwa wa La Liga Barcelona wameitwanga Getafe Bao 6-0 na kuendelea kukaa kileleni wakiwa Pointi 6 mbele ya Atletico Madrid ambao nao waliifunga Deportivo La Coruna 3-0 hapo Jana.
Timu ya 3 ni Real Madrid ambao Leo wako Ugenini kucheza na Las Palmas huku wakiwa Pointi 9 nyuma ya Atletico.
Bao za Barca Jana zilifungwa na Juan Rodriguez, aliejifunga Dakika ya 8, Munir El-Haddard, 19, Neymar, 32 na 51, Messi, 40, na Arda Turan, 57.
Messi pia alikosa Penati katika Dakika ya 11.
Ushindi wa Atletico dhidi ya Deportivo ulipatokana kwa Bao za Saul Niger, Antoine Griezman na Angel Correa.


Mahabiki : 87533
BAO za Barcelona zimefungwa na 
Juan Rodríguez 8' OG •
Munir El Haddadi 19' •
Neymar 32' •
Lionel Messi 40' •
Neymar 51' •
Arda Turan 57' •