Wednesday, March 16, 2016

FULL TIME..UEFA CHAMPIONS LEAGUE: BARCELONA 3 v 1 ARSENAL (Agg 5-1) NEYMAR, MESSI NA SUAREZ WATAMBA NOU CAMP!


MABINGWA Watetezi Barcelona na Bayern Munich Jana Usiku zimefuzu kuingia Robo Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, na kukamilisha idadi ya Timu 8 ya Raundi hiy baada kushinda Mechi zao za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 walizocheza kwao.
Huko Nou Camp Jijini Barcelona Nchini Spain, Barcelona waliinyuka Arsenal 3-1 na kutinga Robo Fainali kwa Jumla ya Mabao 5-1 baada ya pia kushinda Mechi ya Kwanza 2-0.


Barcelona sasa wako njiani kuiga kile kilichofanywa na AC Milan Miaka ya 1989 na 1990 kwa kutwaa UCL mara mbili mfululizo.
Kwa Arsenal huu sasa ni mwisho wa Msimu wao labda wafanye miujiza kwenye Ligi Kuu England ambako wanashika Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City huku Mechi zikibaki 9 kwao.
1-1 mapema kipindi cha pili