Sunday, March 20, 2016

PREMIER LEAGUE: NEWCASTLE UNITED 1 v 1 SUNDERLAND, MITROVIC AIOKOA NEWCASTLE KWAO KWA KUSAWAZISHA BAO DAKIKA ZA MWISHONI!

Mitrovic aisawazishia bao Newcastle kwa kufanya 1-1 dakika za mwishoni
Defoe akishangilia bao lake
Huko Saint James Park, Aleksandar Mitrovic aliiokoa Newcastle kutoka kipigo cha Mahasimu wao Sunderland baada ya kusawazisha kwa Kichwa alipounganisha Krosi ya Georginio Wijnaldum zikiwa zimebaki Dakika 7 Mpira kwisha.
Bao la Sunderland lilifungwa na Jermain Defoe katika Dakika ya 44.
Mbali ya Mechi hii ilikuwa Dabi, hivyo ni ngumu, lakini pia Timu hizi zinafuatana zikiwa juu toka Timu ya Mkiani Aston Villa ambayo ina Pointi 16 na juu wako Newcastle wana Pointi 25 na Sunderland 26.
VIKOSI:
Newcastle:
Elliot, Janmaat, Mbemba, Lascelles, Colback, Sissoko, Shelvey, Townsend, Wijnaldum, Perez, Mitrovic.
Akiba: Anita, Cisse, De Jong, Saivet, Darlow, Taylor, Riviere.

Sunderland: Mannone, Yedlin, Kone, Kaboul, Van Aanholt, Kirchhoff, Borini, M'Vila, Rodwell, Khazri, Defoe.
Akiba: Jones, Cattermole, N'Doye, Pickford, O'Shea, Lens, Toivonen. Referee: Martin Atkinson