Saturday, March 26, 2016

LUKAKU AANZA MCHECHETO KUIHAMA EVERTON, BAYERN, MAN UNITED ZAMWANIA! BABA NAE AUNGA MKONO!

Romelu Lukaku ametoboa waziwazi kutoridhishwa na Klabu yake Everton na kuonyesha nia ya kujiunga na Klabu nyingine ili acheze UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Lukaku, ambae Msimu huu amepachika Mabao 25, yupo kambini na Timu ya Taifa ya Belgium ikijitayarisha kucheza na Portugal Jumanne.
Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea amesema hatua nyingine kwenye Soka lake ni kujiunga na Klabu nyingine ili acheze Mashindano ya Ulaya Msimu ujao kitu ambacho Everton, ambao wapo Nafasi ya 12 kwenye Ligi Kuu England na Pointi 13 nyuma ya Timu ya 4 Man City hawawezi wakikipata Msimu huu.
Huku Baba yake Mzazi akimhimiza ahamie Klabu kubwa kama Bayern Munich na Manchester United, Lukaku amesema hizo ni Klabu ambazo Baba yake anazipenda lakini Wakala wake yupo kazini ambae anashughulikia masuala yake.
Lukaku amehusishwa pia na kurejea Chelsea ambako aliondoka kwa Dau la Pauni Milioni 28 kuhamia Everton Mwaka 2014 lakini mwenyewe ametamka: “Hapana, nitasema hapana kwa hilo. Sina cha kujiridhisha huko. Nilihama na wao wakasonga. Wakatwaa Ubingwa na mimi nikaongeza ubora na sasa tutazame baadae kuna nini!”