Tuesday, March 1, 2016

MAN UNITED WAPATA AHUENI MAJERUHI 3 KATI YA 17 WAREJEA, LAKINI WANA KIBARUA KIGUMU MWEZI HUU WA MACHI- NDANI YA SIKU 19 WANA MECHI 6.

www.bukobasports.comLICHA ya kuwa na Listi ndefu ya Majeruhi waliofikia 17, Manchester United walifanikiwa kushinda Mechi 3 muhimu ndani ya Wiki 1 iliyoisha na kuanzia Jumatano wanaanza mfululizo wa Mechi 6 ndani ya Siku 19.
Wakicheza bila Kepteni wao Wayne Rooney na Mastaa kibao, Wiki iliyopita Man United waliziteketeza Shrewsbury Town kwenye FA CUP, FC Midtyjlland 5-1 kwenye EUROPA LIGI na Juzi Jumapili Arsenal 3-2 kwenye Ligi Kuu England huku Kikosi kikiimarishwa na Wachezaji Chipukizi wakiongozwa na Kinda wa Miaka 18 Marcus Rashford aliepiga Bao 4 katika Mechi 2 zilizopita.

Jumatano wapo tena Old Trafford kuivaa Watford United na safari hii Meneja Louis van Gaal amedokeza kuwa Majeruhi Watatu, Anthony Martial, Chris Smalling na Matteo Darmian, wanaweza kushiriki Mechi hiyo.
Van Gaal pia alidokeza Marouane Fellaini na Antonio Valencia wako karibu kuwa fiti ila Kepteni Rooney bado kidogo.

RATIBA YA MECHI ZA MAN UNITED MWEZI HUU MACHI
Ligi Kuu England

Man United v Watford [Jumatano Machi 2 Saa 23:00]

Ligi Kuu England
West Brom v Man United [Jumapili Machi 6 19:00]

Europa Ligi – Raundi ya Mtoano Timu 16
Liverpool v Man United [Alhamisi Machi 10 23:05]

FA Cup – Robo Fainali
Man United v West Ham [Jumapili Machi 13 19:00]

Europa Ligi – Raundi ya Mtoano Timu 16
Man United v Liverpool [Alhamisi Machi 17 21:00]

Ligi Kuu England
Man City v Man United [Jumapili Machi 20 19:00]