Friday, March 4, 2016

MASHINDANO YA DIAMOND LEAGUE KUFANYIKA BARANI AFRIKA

Mji wa Rabat utakuwa wa kwanza Afrika kuandaa mashindano ya riadha ya Diamond League, utakapokuwa mwenyeji wa mashindano hayo baadaye mwaka huu.
Jiji la New York hata hivyo limeondolewa kutoka kwenye mashindano hayo
Rabat, mji mkuu wa Morocco, utaandaa mashindano ya tatu ya msimu huu mnamo 22 Mei.
Rais wa Shirikisho la riadha duniani (IAAF) Lord Coe amesema kupitia taarifa: “Tuna furaha sana kupeleka mashindano haya makuu ya riadha hadi kwenye bara jingine.”
Waandalizi wa mashindano hayo jijini New York wamesema watajaribu kuandaa mashindano mengine badala ya Diamond League.
Marekani sasa imebaki na jiji moja pekee linaloandaa mashindano ya Diamond League, mji wa Eugene, Oregon.
Morocco imewahi kuandaa mashindano ya IAAF zamani, yakiwemo mashindano ya mabara ya 2014 mjini Marrakech.