Friday, March 11, 2016

McCLAREN ATIMULIWA KLABUNI NEWCSTLE UNITED, BENITEZ YU NJIANI....

Steve McClaren amefukuzwa kazi kama Meneja wa Newcastle United.
McClaren, mwenye Miaka 54, ametolewa kwenye wadhifa huo baada ya Miezi 9 huku Newcastle ikiwa Nafasi ya 19 kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni nafasi 1 tu juu ya Timu ya mkiani Aston Villa.
Tangu McClaren atwae wadhifa huo mwanzoni mwa Msimu huu Newcastle imeshinda 7 tu kati ya 30.
Mechi ya mwisho kwa McClaren ilikuwa Jumamosi iliyopita Newcastle wakiwa kwao St James Park na kupigwa 3-1 na Bournemouth ikiwa ni kipigo chao cha 5 katika Mechi 6 zilizopita.
Habari za ndani ya Newcastle zinamtaja Rafael Benitez, Meneja wa zamani wa Chelsea, Liverpool na Real Madrid, kumrithi McClaren.
Inaaminika Muhispania huyo huenda akateuliwa haraka na kutwaa wadhifa kabla Newcastle haijasafiri kwenda huko King Power Stadium Jumatatu Usiku kucheza na Leicester City.