Wednesday, March 2, 2016

MICHEL PLATINI AKATA RUFAA DHIDI YA MARUFUKU

WWW.BUKOBASPORTS.COMMichel Platini, aambaye ni kapteni wa zamani wa Ufaransa anataka kugeuza uamuzi wa shirikisho la soka duniani FIFA kumpiga marufuku ya miaka sita kwa kupokea malipo ya dola ilioni mbili kutoka kwa Sepp Blatter.
Ni hatua ya mwisho kwa Michel Platini, ambaye bado ni mkuu rasmi wa UEFA ukisubiriwa uamuzi wa rufaa hiyo.
Ameiomba mahakama hiyo ya Uswizi kutupilia mbali marufuku hiyo ya miaka sita iliyopunguzwa hivi karibuni na FIFA kutoka miaka 8.
Na anataka uamuzi utolewe kabla ya michuano ya ubingwa wa Ulaya nchini Ufaransa inayoanza Juni.
Alihusika pakuu katika uandalizi wa mashindano hayo nyumbani na ana hamu kubwa kuyahudhuria.
Ameendelea kusisitiza kuwa pesa hizo za dola milioni mbili alizopewa na mkuu wa zamani wa FIFA zilikuwa ni malipo ya kazi ya ushauri aliotoa miaka tisa iliyopita na ni za halali kwasabau kulikuwana makubaliano ya mdomo.
Sepp Blatter, anakabiliwa na marufuku ya miaka sita kuhusu suala lilo hilo anatarajiwa pia kuwasilisha kesi yake mbele ya mahakama hiyo inayotoa uamuzi wa mwisho kuhusu mizozo aina hiyo.

Aliyekuwa naibu wa Michel Platini katika UEFA, Gianni Infantino amechaguliwa rais wa FIFA ijumaa iliyopita hatua iliyoacha pengo katika uongozi wa shirikisho hilo la soka Ulaya miezi michache kabla ya kuidhinishwa kwa mara ya kwanza michuano yake.