Thursday, March 24, 2016

MKONGWE WA SOKA LEJENDARI JOHAN CRUYFF AFARIKI DUNIA

LEJENDARI wa Holland Johan Cruyff amefariki Dunia kwa ugonjwa wa Kansa akiwa na Umri wa Miaka 68.
Kruyff, ambae mara 3 aliwahi kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, aliiongoza Holland kufika Fainali ya Kombe la Dunia Mwaka 1974 na pia kuwa Meneja wa Barcelona kwa Miaka Minane.
Mwezi Oktoba Mwaka Jana, Cruyff, aliewahi pia kuzichezea Klabu za Ajax na Barcelona, alitoboa kuwa amekumbwa na Kansa ya Mapafu lakini Mwezi uliopita alitamka kuwa anaongoza 2-0 katika vita yake ya kupigana na Kansa hiyo. Cruyff ni Lejendari wa ukweli kabisa na aliiwezesha Ajax kutwaa Ubingwa wa Ulaya mara 3 mfululizo kuanzia 1971 hadi 1973 na alikuwa ndie nguzo kubwa ya Holland iliyofungwa Fainali ya Kombe la Dunia ya Mwaka 1974 na Germany huku wakitumia Staili maarufu ya ‘Soka Kamili’, ‘Total Football’.
Kisha akajiunga na Klabu ya Barcelona kwa Dau la Dunia wakati huo na kuiwezesha kutwaa Ubingwa wao wa kwanza wa Ulaya Mwaka 1992 na pia kutwaa Ubingwa wa La Liga mara 4 mfululizo kuanzia 1991 hadi 1994. 

Mtoto wa Johan Cruyff, Jordi Cruyff, aliwahi kuichezea Manchester United kati ya 1996 mpaka 2000.

Miongoni mwa Watu wa kwanza kabisa kutuma rambrambi ni Mchezaji Bora Duniani wa sasa Lionel Messi ambae alituma ujumbe kwenye Akaunti yake ya Twitter ukisema: “RIP Johan Cruyff. Urithi wako utaishi daima milele.”