Thursday, March 17, 2016

MONGELLA AANZA NA KIPINDIPINDU JIJINI MWANZA

Na. Atley Kuni- Afisa habari Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema ifikapo tarehe 30. Mei, 2016 endapo viongozi wa Wilaya za mkoa huo watakuwa bado wanakabiliwa na Ugonjwa wa Kipindupindu katika wilaya zao basi wajiandae kuwajibika.
Alitoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kikao cha kujitambulisha kwenye ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mwanza mara baada yakuwasili mkoani humo na kuanza kazi mara moja.
Mongella alisema moja ya jambo lililonikera nikuona mkoa huo bado unakabiliwa na adha ya kipindupindu huku Wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wataalam wakiwa hawana mipango madhubuti yakutokomeza janga hilo “sasa tutaanza Operesheni maalum ijulikanayo Tukomeza Kipindupindu Mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 01 Aprili,2016 na hatutakuwa na simile na yeyote atakayetukwamisha” alisema na kusisitiza “Nina Machinery zote kwa nini nishindwe?