Saturday, March 26, 2016

MWANAHISA MKUU ARSENAL, ALISHER USMANOV ASEMA WENGER BADO ANAHITAJIKA KLABUNI!

MMOJA wa Wanahisa wakubwa wa Arsenal, Alisher Usmanov, amedai Klabu hiyo bado inamhitaji Arsene Wenger.
Usmanov, mwenye Hisa Asilimia 30.05% ya Kampuni inayoimiliki Arsenal, amedai Wenger anapaswa kuhusishwa na mchakato wa kumteua Mrithi wake endapo ataamua kuondoka.
Mfanyabiashara huyo wa Urusi amesema: “Klabu lazima iibakishe alama yake kubwa na mali yake muhimu ambayo ni Arsene Wenger!”
Lakini licha ya kumsapoti Wenger, Usmanov pia amedai Arsenal inasakamwa na kushindwa kwao kwa Miaka mingi kutwaa Ubingwa wa Ligi na pia kutamka waziwazi kuwa Msimu huu nao hawatatwaa Ubingwa.

Usmanov ameeleza: “Wenger ni Kocha mzuri na Arsenal inapaswa kumpa nafasi kwenye mchakato wa Mrithi wake akiamua kuondoka.”
Akiongea kwenye Kipindi cha TV ya Rossiya24, Usmano alitamka: “Kufeli kumeisakama Arsenal kwa Miaka mingi sasa, hawawezi kuwa tena Mabingwa wa England. Hilo limeleta kutofurahishwa kwa nafasi ya Wenger kama Meneja!”

DONDOO MUHIMU:
-Klabu ya Arsenal inamilikiwa na Kampuni ya Arsenal Holdings, PLC ambayo Wanahisa wake wakubwa ni Mmarekani Stan Kroenke, mwenye Hisa 66.64% na Mrusi wa Uzbekistan Alisher Usmanov, mwenye Asilimia 30.05% 

 
Msimu huu, tayari Arsenal wameshatupwa nje ya UEFA CHAMPIONS LIGI na pia FA CUP, Kombe ambalo walilitwaa kwa Misimu Miwili mfululizo iliyopita.
Hivi sasa Arsenal wapo Nafasi ya 3 kwenye Ligi Kuu England wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Leicester City huku Mechi zikizidi kuyoyoma.
Wenger, ambae amekuwa Arsenal tangu 1996, alitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England kwa mara ya mwisho Mwaka 2004.