Sunday, March 27, 2016

NAVY KENZO WATUA BUKOBA, TAYARI KWA SHOW YAO USIKU HUU LINA'S NIGHT CLUB

Na Faustine Ruta, Bukoba
Wasanii wanaounda kundi la Navy Kenzo, Nahreel na Aika leo wametua Bukoba ikiwa ni mwendelezo wao wa  "Kamatia Chini lights up Tour" ambapo usiku huu watashusha show yao ya Nguvu kwenye Ukumbi wa Burudani wa Lina's Night uliopo Bukoba Mjini. Wasanii hao wanaletwa hapa Mjini Bukoba kupitia kampuni ya Sleek Events ya Jijini Mwanza.
Msanii Aika akishuka kwenye ndege leo hii kwenye Uwanja wa Ndege Mjini Bukoba
Nahreel Tayari kwa Kazi usiku huu Lina,s Club
bukobasports.comKaribu Bukoba....
Picha ya Pamoja na Wadau wao
Msanii Aika akijiself

Wadau wakipata picha ya pamoja na wasanii wa Kundi la Navy Kenzo
Furaha baada ya kutua mjini Bukoba.
Kushoto ni Mr. Tega Jasson Mkurugenzi wa Sleek Events akitokelezea kwenye picha ya pamoja na msanii Aika, Faustine Ruta wa Bukobasports.com na kulia ni Bwogi.