Sunday, March 20, 2016

FULL TIME: PREMIER LEAGUE, MANCHESTER CITY 0 v 1 MANCHESTER UNITED, KINDA RASHFORD AACHA KILIO ETIHAD LEO KWA KUIPA UNITED USHINDI!

1-0 Furaha tupu kwa Rashford!Rashford alipotingisha nyavu za City leo kwenye mechi yao ya Dabi iliyomalizika kwa bao 1-0, United wakiibuka kidedea.Marcus Rashford Leo aliifungia Manchester United Bao pekee na la ushindi kwenye Dabi ya Jiji la Manchester walipowatungua Manchester City 1-0 na kuweka hai matumaini yao ya kumaliza ndani ya 4 Bora.
Bao la Rashford lilifungwa Dakika ya 15 baada kupokea Pasi murua ya Juan Mata na kumpiga chenga Sentahafu wa City Demichelis na kupiga shuti kifundi kumzidi akili Kipa Joe Hart.
Bao hilo limeweka Rekodi mpya huko England kwa Rashford, ambae ana Miaka 18, kufunga Bao kwenye Dabi akiwa Kijana mdogo kabisa. 
Bao...
Man United wapo Nafasi ya 6 wakiwa Pointi sawa na Timu ya 5 West Ham ambao wamewazidi Bao 1 tu huku City wakiwa Nafasi ya 4 wakiwa Pointi 1 tu mbele.
Rooney akiuchiki mtanange kusawasawa  leo kwenye DabiAsante kutoka kwa MashabikiMwenyekid Ed Woodward akiwa na mmiliki wa City Sheikh Mansour Bin Zayed leoMarcus ndie aliyeipa ushindi leo UnitedRashford akishangilia bao lakeSilva akiendesha mpira huku akinyemelewa na Juan MataMeneja Van GaalKipa Joe Hart akiondoshwa nje mara baada ya kuumiaNje!Joe akijiuguzaTofauti ilitokea,,,Rashford akiwekewa vikwazochupuchupu!Wayne RooneyMashabiki wa City wakiondoshwa na Askari Uwanjani!Mwishoni mambo hayakwenda safi kwa MashabikiVIKOSI:
Manchester City wanaoanza XI:
Hart, Sagna, Demichelis, Mangala, Clichy, Toure, Fernandinho, Jesus Navas, Silva, Sterling, Aguero
Man City akiba: Zabaleta, Fernando, Kolarov, Caballero, Bony, Iheanacho, Manu Garcia
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Schneiderlin, Lingard, Mata, Martial, Rashford
Man Utd akiba: Depay, Januzaj, Romero, Valencia, Fellaini, Schweinsteiger, Fosu-Mensah