Sunday, March 6, 2016

FULL TIME: SIMBA SC 2 v 0 MBEYA CITY, MWIKO WAVUNJWA TAIFA LEO! SIMBA KILELENI!

Simba Leo imechukua usukani wa Ligi Kuu Vodacom, VPL, kwa kuifunga Mbeya City Bao 2-0 katika Mechi iliyochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu umewafanya Simba wawe vinara wa VPL wakiwa na Pointi 48 kwa Mechi 21 wakifuatiwa na Yanga wenye Pointi 47 kwa Mechi 20 na wa 3 ni Azam FC wenye Pointi 47 kwa Mechi 20 lakini wako nyuma kwa uhafifu wa Magoli.
Bao za Simba hii Leo zilifungwa zote Kipindi cha Pili na Daniel Lyanga, Dakika ya 75, na Ibrahim Ajib, Dakika ya 90.

VPL itaendelea tena hapo Jumanne wakati Yanga wakiwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Ndugu zao kutoka Tanga, African Sports.
Jumatano zipo Mechi 5 ikiwemo ile ya Mtibwa Sugar na Azam FC huko Manungu, Morogoro na Simba watacheza Alhamisi na Jijini Dar es Salaam na Ndanda FC.
Mbeya City wanacheza 4-4-2
Simba nao wanacheza mfumo wa 4-4-2