Friday, March 11, 2016

RAFAEL BENITEZ MENEJA MPYA NEWCASTLE UNITED!

NEWCASTLE imemteua Meneja wa zamani wa Liverpool, Chelsea na Real Madrid, Rafa Benitez, kuwa Meneja wao mpya.
Ijumaa Asubuhi, Newcastle ilimtimua Steve McClaren baada ya matokeo mabove na Leo kumteua Benitez ambae alitimuliwa na Real madrid Mwezi Januari.
Benitez amesaini Mkataba wa Miaka Mitatu na Newcastle ambayo iko Nafasi ya 19 kwenye Ligi Kuu England.
Gemu ya kwanza kwa Benitez itakuwa Ugenini Jumatatu Usiku na Vinara wa Ligi Kuu England Leicester City huko King Power Stadium.