Sunday, March 20, 2016

RIPOTI ZAANIKA WAZI KUWA JOSE MOURINHO AMEISHASAINI £15 MKATABA WA AWALI NA MAN UNITED

José Mourinho amedaiwa kuwa tayari ameshaini Mkataba wa awali ili ajiunge na Manchester United na atalipwa Fidia ya Pauni Milioni 15 ikiwa hatateuliwa kuwa Meneja wa Manchester United ifikapo Juni 1.
Mourinho amekuwa hana kibarua tangu atimuliwe Chelsea Mwezi Desemba lakini amekuwa akihusishwa sana na kumrithi Louis va Gaal huko Man United.
Kwa mujibu wa Gazeti la Spain, El Pais, chanzo kutoka kwa Wakala wa Mourinho, Kampuni ya Jorge Mendes, imethibitisha kuwa Mreno huyo mwenye Miaka 53 alisaini Mkataba wa awali na Man United tangu Mwezi uliopita.

Ripoti ya Al Pais imesema ikiwa Man United haitasaini Mkataba kamili na Mourinho ifikapo Mei 1 basi Mourinho atalipwa Pauni Milioni 5 na ikifika Juni 1 kama pia haujasainiwa Mourinho atalipwa Pauni Milioni 10 nyingine.
Gazeti hilo limedai kipengele cha Mkataba kusainiwa na ikiwa hautasainiwa Mourinho alipwe Fidia kimeingizwa kwa sababu baadhi ya Viongozi wa juu wa Man United, wakiwemo Sir Alex Ferguson na Sir Bobby Charlton, hawaridhishwi kuwa Mourinho ndio chaguo linalofaa kumrithi Louis van Gaal.Harry Kane kuletwa Old Trafford na Jose Mourinho