Thursday, March 10, 2016

SIMBA YARUDI KILELENI LEO, MBEYA CITY YAPANDA JUU IPO NAFSI YA 9

MATOKEO
Alhamisi Machi 10

Simba 3 vs Ndanda FC 0
Mbeya City 2 vs Stand United 0

VPL, Ligi Kuu Vodacom, iliendelea Leo kwa Mechi 2 na Simba kurejea kileleni wakiwa Pointi 1 mbele ya Mabingwa Watetezi Yanga lakini wao wamecheza Mechi 1 zaidi.

Simba, wakicheza Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wameichapa Ndanda FC Bao 3-0 kwa Bao za Mwinyi Kazimoto na 2 za Kipindi cha Pili za Mchezaji wa Kimataifa wa Uganda Hamisi Kiiza.

Bao hizo 2 za Kiiza zimemfanya ampite Straika wa Yanga Amisi Tambwe kwa Bao 1 na kuongoza Listi ya Mfungaji Bora wa VPL yeye sasa akiwa na Bao 18.

Huko Sokoine Jijini Mbeya, Wenyeji Mbeya City wameicharanga Staind United Bao 2-0 kwa Bao za Raphael Daudi na Haruna Shamte.

LIGI KUU VODACOM
RATIBA
Jumamosi Machi 12

Mtibwa Sugar v JKT Ruvu

Jumapili Machi 13
Majimaji FC v Stand United
Kagera Sugar v Coastal Union
Simba v Tanzania Prisons
Mgambo JKT v Mwadui FC

Jumatatu Machi 14
African Sports v Mbeya City