Tuesday, March 15, 2016

TAARIFA KUTOKA KLABU YA SIMBA

Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko taarifa ya kifo na mchezaji wake wa zamani Ayuob Mohammed(captain)
Kifo hicho kimetokea leo asubuhi nyumbani kwake Mwananyamala B.na mazishi yake yanatarajiwa kuwa kesho alasiri huko huko Mwananyamala hapa jijini Dar es salaam
Captain Ayuob licha ya kuichezea Simba.enzi hizo ikiitwa Sunderland.pia aliichezea kwa muda mrefu timu ya taifa ya Tanganyika huku akiwa nahodha wa timu zote.Sunderland na Tanganyika.
Captain Ayuob anakumbukwa vizuri wakati akiwa kocha na marehemu Paul West Gwivaha kwa pamoja waliiwezesha Simba kuifunga timu ya Mufurila wonderes ya 5-0 kwao nchini Zambia baada ya timu hiyo kuifunga Simba 4-0 hapa nchini kwenye mchezo wa awali.
Ikumbukwe historia hiyo haijawahi kuvunjwa na klabu yoyote ktk historia ya michuano ya klabu bingwa barani afrika.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.amiiin
Wakati huo huo klabu inawaalika wanahabari kwenye mkutano wake na wanahabari hapo kesho kuanzia saa sita mchana klabuni mtaa wa msimbazi jijini Dar es salaam. Kwenye mkutano huo kocha wa Simba Jackson Mayanja pia atapata fursa ya kuzungumzia maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya coastal union ya Tanga.
Mchezo utakaofanyika mwishoni mwa wiki jijini Tanga.

Imetolewa na
Haji S Manara
Mkuu wa habari wa Simba

Simba nguvu moja