Monday, March 28, 2016

TFF YATHIBITISHA KUJITOA KWA CHAD KATIKA MICHUANO YA AFCON 2017

Shirikisho la Soka nchini TFF limethibitisha taarifa yetu ya awali kwamba timu ya Taifa ya Chad ‘Les Sao’ (pichani) imejiondoa katika michuano ya kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) itakayofanyika mwaka 2017 nchini Gabon. Tovuti ya TFF inasema kwamba taarifa ya kujitoa kwa Chad imetolewa na Shirikisho la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) leo baada ya Les Sao kuandika barua ya kujitoka katika mashindano hayo ikiwa katika kundi G pamoja na timu za Tanzania, Nigeria na Misri. Chad ilitarajiwa kucheza kesho Jumatatu dhidi ya Tanzania katika uwanja wa Taifa