Monday, March 14, 2016

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: PATASHIKA TENA JUMANNE, MAN CITY, ATLETICO, PSV NA KIEV NANI ROBO FAINALI? JUMATANO NGOMA NZITO NOU CAMP, ARSENAL KULIPA KISASI KWA BARCA? BAYERN, JUVE NANI KUSONGA?

UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI itakamilisha idadi ya Timu 8 kucheza Robo Fainali baada ya Wiki iliyopita 4 kupatikana na Jumanne na Jumatano kutoa Timu nyingine 4.
Jumanne Usiku zipo Mechi mbili kati ya Atletico Madrid na PSV Eindhoven huko Vicente Calderon Jijini Madrid baada ya Timu hizi kutoka 0-0 kwenye Mechi ya kwanza na nyingine ni ile itakayopigwa Etihad Jijini Manchester huku Man City wakiwa kifua mbele baada ya kuinyuka Dynamo Kiev 3-1 katika Mechi ya kwanza.

TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI:
-Real Madrid
-VfL Wolfsburg
-Paris St Germain
-Benfica

Mechi nyingine 2 zitapigwa Jumatano Usiku na ile tamu kabisa ni ile ya Nou Camp wakati Barcelona watarudiana na Arsenal huku wao wakiwa washindi wa 2-0 baada ya Mechi ya kwanza iliyochezwa Emirates.
Nyingine ni huko Allianz Arena Jijini Munich huku Bayern Munich na Juventus zikiwa zimetoka Sare ya 2-2 kutoka Mechi ya kwanza iliyochezwa Turin Nchini Italy.