Monday, March 7, 2016

UEFA CHAMPIONS LIGI: REAL vs AS ROMA, WOLFSBURG v KAA GENT...NANI KUFUZU ROBO FAINALI KESHO JUMANNE?

RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano
Mechi zote Saa 4 Dakika 45 Usiku
Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza

JUMANNE 8 MAR 2016
Real Madrid v AS Roma [2-0]
VfL Wolfsburg v KAA Gent [3-2]

JUMATANO 9 MAR 2016
20:00 Zenit St Petersburg v Benfica [0-1]
Chelsea v Paris St Germaine [1-2]
Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, zitaanza Jumanne Usiku kwa Mechi mbili ambazo Real Madrid na VfL Wolfsburg wapo katika nafasi nzuri kutinga Robo Fainali baada ya kushinda Mechi za Ugenini.
Real Madrid, ambao Jumanne wako kwao Santiago Bernabeu kurudiana na AS Roma, walishinda Mechi ya Kwanza 2-0 wakati VfL Wolfsburg waliichapa KAA Gent na Kesho Jumanne wapo kwao huko Germany.
Jumatano pia zipo Mechi 2 za Marudiano ambapo Zenit Saint Petersburg wapo kwao Urusi huku wakiwa nyuma kwa Bao 1-0 walipofungwa Mechi ya Kwanza na Benfica.
Uwanjani Stamford Bridge, Jijini London, Chelsea, baada ya kuchapwa 2-1 na Paris St Germaine huko Paris, France, wanahitaji ushindi wa 1-0 au zaidi ili wafuzu.
Wiki ijayo, Raundi ya Mtoano ya Timu 16 itakamilika kwa Mechi 4.
REFA: A Mateu Lahoz (Spain)

UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16
Marudiano

JUMANNE 15 MAR 2016
Atletico Madrid v PSV Eindhoven [0-0]
Man City v Dynamo Kiev [3-1]
 

JUMATANO 16 MAR 2016
Barcelona v Arsenal [2-0]
Bayern Munich v Juventus [2-2]