Thursday, March 10, 2016

UEFA EUROPA LEAGUE: LEO ALHAMISI NI LIVERPOOL vs MAN UNITED IKIWA NI MARA YA KWANZA KUKUTANA MASHINDANO YA ULAYA! BORUSSIA DORTMUND vs TOTTENHAM HOTSPUR

ALHAMISI Usiku huko Anfield, Mahasimu wakubwa wa England, Liverpool na Manchester United, watapambana kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA EUROPA LIGI.
Hii ni Mechi ya 195 kwa Klabu hizi kupambana lakini hii itakuwa ni mara ya kwanza kwao kupambana kwenye Mashindano ya UEFA Barani Ulaya.

Licha ya Kombe hilo kudharauliwa na Wadau na kutukuzwa UEFA CHAMPIONS LIGI, Lakini kwa Klabu hizi ambazo zipo Nafasi za 6, Man United, na ya 7, Liverpool, kwenye Ligi Kuu England na hivyo kupunguza nafasi zao za kucheza UCL Msimu ujao, kulitwaa Kombe hili kutawapa fursa ya kucheza UCL Msimu ujao.

KUKUTANA:
-Hii ni mara ya kwanza kwa Klabu hizi kukutana kwenye Mashindano ya UEFA.
-Liverpool na Man United zimekutana mara 166 kwenye Ligi na Man United kushinda mara 67 na Liverpool mara 55
-Kwenye Vikombe huko England wamecheza mara 18 huku Man United wakiongoza kwa kushinda mara 11 na Liverpool mara 7
-Katika Mechi 4 zilizopita, Man United wameshinda mara zote chini ya Meneja wao Louis van Gaal


REFA: Carlos Velasco Carballo (Spain)
EUROPA LEAGUE - Raundi ya Mtoano ya Timu 16

MUDA:
21:00 FC Shakhtar Donetsk v RSC Anderlecht
21:00 FC Basel 1893 v Sevilla FC
21:00 Borussia Dortmund v Tottenham Hotspur
21:00 Fenerbahce v SC Braga
23:05 Villarreal CF v Bayer 04 Leverkusen
23:05 Athletic Club v Valencia CF
23:05 Liverpool v Manchester United
23:05 Sparta Prague v Lazio