Wednesday, March 16, 2016

UEFA EUROPA LEAGUE: LEO ALHAMISI USIKU: MAN UNITED NA SPURS KWENYE PATASHIKA KUTAFUTA NAFASI ZA KUWABANA WENZAO, MAN UNITED v LIVERPOOL, SPURS v BORUSSIA DORTMUND

ALHAMISI Usiku ni Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UEFA EUROPA LIGI na Manchester United na Tottenham zote ziko Viwanja vya Nyumbani kwao vikidaiwa kushinda kwa ushindi wa kishindo ili kutinga Robo Fainali kufuatia vipigo katika Mechi zao za kwanza.
Tottenham, maarufu kama Spurs, wako kwao White Hart Lane Jijini London kurudiana na Vigogo wa Germany Borussia Dortmund ambao walishinda Mechi ya kwanza 3-0 na hivyo Spurs wanapaswa kushinda 4-0 ili kusonga.
Nako huko Old Trafford ni marudiano ya Mahasimu wakubwa wa Soka la England ambapo Man United wanatakiwa waifunge Liverpool 3-0 ili wasonge baada ya kutandikwa 2-0 Wiki iliyopita huko Anfield kwa Bao za Penati ya Daniel Sturridge na Roberto Firmino. Takwimu muhimu:
-Man United na Liverpool zimekutana Jumla ya Mechi 166 za Ligi na Man United wanaongoza kwa ushindi wa Mechi 67 kwa 55 za Liverpool na kwenye Mechi za Vikombe vya England walivyokutana, Man United wameshinda 11 na Liverpool Mechi 7 tu.
-Uwanjani Old Trafford, Man United wameitandika Liverpool katika Mechi 4 zilizopita zote zikiwa za Ligi na kushinda Mechi 9 kati ya 10 zilizopita Uwanjani Old Trafford wakipambana na Liverpool.