Monday, March 7, 2016

VAN GAAL ALAUMU REFA NYEKUNDU YA MATA

Kwa mujibu wa Meneja wa Man United, Louis van Gaal, Refa Mike Dean alipaswa kujua Juan Mata ni Mchezaji wa aina gani kabla ya kumpa Kadi Nyekundu huko The Hawthorn iliyowafanya Man United wacheze Mtu 10 kuanzia Dakika ya 25 na hatimae kufungwa 1-0 na West Brom. Refa wa Mechi hiyo Mike Dean, ambae ndie kinara wa Kadi Nyekundu nyingi huko England, alimpa Kadi ya Njano Mata kwa kuizuia Frikiki ya Darren Fletcher, Mchezaji wa zamani wa Man United, na Dakika 3 baadae Mata akapewa Kadi ya Njano ya Pili kwa kumkwatua Fletcher.
Kisheria, Refa Dean hakukosea lakini Van Gaal amesema: "Refa anapaswa kumjua Mtu. Mata hajawahi kumuumiza Mpinzani."
Mata, Mchezaji wa Kimataifa wa Spain mwenye Miaja 27, hajawahi kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Van Gaal ameeleza: "Refa ana haki kutoa Kadi mbili lakini anapaswa kumtambua mkosaji ni Mtu wa aina gani!"