Monday, March 21, 2016

VAN GAAL ATEGEMEA MAN UNITED KUMALIZA MSIMU HUU IKIWA NDANI YA 4 BORA, KANE ASEMA LEICESTER AKITELEZA TU TUNAMALIZA MCHEZO NA KUTWAA UBINGWA!

WAKATI Meneja wa Manchester United Louis van Gaal anategemea Timu yake kumaliza ndani ya 4 Bora ya BPL, Ligi Kuu England, Straika wa Tottenham Harry Kane anaamini Leicester City hawawezi kushinda Gemu zao zote 7 zilizobaki na kutwaa Ubingwa.
LOUIS VAN GAAL
Baada Tineja Marcus Rashford Jana kufunga Bao pekee la ushindi wakati Man United inaipiga Man City 1-0 katika Dabi ya Jiji la Manchester kwenye Mechi ya BPL iliyochezwa Etihad, Meneja wa Man United Louis van Gaal watamaliza ndani ya 4 Bora ya Ligi hiyo na kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao.
Van Gaal alisisitiza umuhimu wa kulikata pengo lao na City, ambao wako Nafasi ya 4, kuwa Pointi 1 na alisema: “Ilikuwa muhimu kushinda. Nilisema mapema lazima tushinde, tupunguze pengo na tumefanya hivyo na sasa nina furaha na fahari kubwa kama Meneja!”
Aliongeza: “Tuna Mechi nyingi za Nyumbani kuliko Ugenini na kawaida Nyumbani hatupotezi na hivyo tuna nafasi!”

HARRY KANE
STRAIKA wa Tottenham Hotspur Harry Kane anaamini wapinzani wao katika mbio za Ubingwa, Leicester City, hawatashinda Mechi zao zote 7 zilizobaki za BPL.
Leicester wanaongoza BPL wakiwa Pointi 5 mbele ya Tottenham huku wote wakibakisha Mechi 7 kumaliza Ligi.
Jana Tottenham waliifunga Bournemouth na Harry Kane kupiga Bao 2 kati ya hizo na kumfanya afikishe Bao 21 kwenye BPL akiongoza katika Ufungaji na kufuatiwa na Jamie Vardy wa Leicester mwenye 19.
Kane anaamini pengo la Pointi 5 na Leicester si kubwa kwani Timu hiyo chini ya Meneja Claudio Ranieri itapata presha na kupoteza Pointi.
Alipoulizwa kama itabidi Tottenham washinde Mechi zao zote zilizobaki ili watwae Ubingwa, Kane alijibu: “Sidhani. Zipo Pointi nyingi za kugombewa na Leicester watapoteza tu na wanamaliza Mechi zao 3 za mwisho na Timu ngumu!”