Wednesday, March 16, 2016

VICENT KOMPANY KUIKOSA DABI YA MANCHESTER JUMAPILI!

KEPTENI wa Manchester City Vincent Kompany ataikosa Dabi ya Manchester itakayochezwa Jumapili huko Etihad kati ya Timu yake na Mahasimu wao wakubwa Manchester United katika Mechi ya Ligi Kuu.
Jana Kompany aliumia Musuli za Mguuni Uwanjani Etihad wakati City ikirudiana na Dynamo Kiev kwenye Mechi ya Marudiano ta Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LIGI waliyotoka 0-0 na wao kutinga Robo Fainali kwa vile walishinda 3-1 huko Ukraine.
Kepteni huyo alilazimika kutolewa nje ta Uwanja muda mfupi baada Mechi na Kiev kuanza baada kuumia kwa mara nyingine tena Musuli za Mguuni ambalo ni tatizo lilokuwa likimzonga kwa Miaka kadhaa sasa.
Kompany alirejea Uwanjani Mwezi uliopita baada ya kupata tatizo hili hili kwenye Mechi ya Desemba 26 dhidi ya Sunderland.
Jana Meneja wa City Manuel Pellegrini alithibitisha kurudi tena kwa tatizo la Kompany ambalo sasa litamweka nje si chini ya Mwezi mmoja.
Hii ni mara ya 12 kwa Kompany kupata tatizo hilo hilo na Msimu huu ni mara ya 3.
Jana nafasi ya Kompany ilizibwa na Eliquim Mangala lakini kwenye Mechi hiyo hiyo City walipata pigo jengine baada Sentahafu wao mwingine Nicholas Otamendi kuumia na kutolewa nje na nae yupo hatarini kuikosa Dabi ya Jumapili.
Dabi hii ya Manchester itachezwa huku kila Timu ikikosa Kepteni wake kwani nao Man United hawatakuwa nae Wayne Rooney ambae yuko nje kwa Wiki kadhaa sasa akiuguza Goti lake.