Wednesday, March 9, 2016

VPL: COASTAL, JKT RUVU ZASHINDA, KAGERA SUGAR YAAMBULIA SARE TENA!! ALHAMISI NI SIMBA v NDANDA, MBEYA CITY v STAND UNITED!

VPL-LIGI KUU VODACOM
Matokeo:
Jumatano Machi 9

Tanzania Prisons 1 vs Kagera Sugar 1
Coastal Union 1 vs Mgambo JKT 0
Mwadui FC 0 vs Majimaji FC 0
JKT Ruvu 2 vs Toto African 0

VPL, Ligi Kuu Vodacom, iliendelea Leo kwa Mechi 4 katika Viwanja mbalimbali.
Huko Mkwakwani, Tanga, Coastal Union iliwatungua wenzao wa Tanga, Mgambo JKT, Bao 1-0 wakati huko Mbeya, Tanzania Prisons na Kagera Sugar zikitoka Sare ya 1-1 na Sare nyingine ilikuwa ya 0-0 huko Shinyanga kati ya Mwadui FC na Majimaji FC.
Jijini Dar es Salaam, JKT Ruvu iliwachapa Toto African Bao 2-0.
VPL itaendelea kwa Simba kucheza Alhamisi Jijini Dar es Salaam na Ndanda FC wakati Siku hiyo hiyo huko Sokoine Jijini Mbeya ni Mbeya City na Staind United.

LIGI KUU VODACOM
Ratiba
Alhamisi Machi 10

Simba vs Ndanda FC
Mbeya City vs Stand United