Tuesday, March 8, 2016

WACHEZAJI WA CHELSEA WAJIFUA KUJIWEKA SAWA NA MCHEZO WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE JUMATANO NA PSG. JOHN TERRY KUIKOSA MECHI HIYO!

Radamel Falcao
Nahodha wa Chelsea John Terry ataikosa Mechi muhimu ya marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, dhidi ya Paris St Germaine Uwanjani Stamford Bridge Jumatano Usiku ambayo wanapaswa kupindua kipigo cha 2-1 ili kutinga Robo Fainali.
Terry hajaichezea Chelsea Mechi 5 zilizopita baada ya kuumia kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Mwezi uliopita walipoichapa Newcastle 5-1.


Kumkosa Terry ni pengo kwa Chelsea ambao inabidi wamchunge mno Straika hatari wa PSG Zlatan Ibrahimovic ambae anasaka Bao 1 tu kufikia Bao 50 kwenye Mechi za Ulaya na kuwa Mtu wa 14 kutimiza idadi hiyo.
Lakini Chelsea watapata ahueni kidogo kwani Straika wao Diego Costa, ambae aliikosa Sare ya Wikiendi ya 1-1 na Stoke City kutokana na maumivu, sasa yuko fiti kuivaa PSG.
Huu ni Msimu wa 3 mfululizo kwa Chelsea na PSG kukutana kwenye hatua za Mtoano za UCL na kila Msimu Timu moja imefuzu kwa mgongo wa Goli za Ugenini.

VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Chelsea:
Courtois; Azpilicueta, Ivanovic, Cahill, Kenedy; Mikel, Fabregas; Hazard, Oscar, Willian; Diego Costa
Paris Saint-Germain: Trapp; Van Der Wiel, Luiz, Silva, Maxwell; Matuidi, Verratti, Motta; Moura, Ibrahimovic, Di Maria
REFA: Felix Brych (Germany)