Monday, March 14, 2016

WAZIRI Mkuu Majaliwa atembelea Kambi ya utenganisho ya wakimbizi ya Mwisa inayosimamiwa na Jeshi la Magereza

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB) alipotembelea Kambi Maalum ya Mwisa inayohifadhi Wakimbizi kutoka nchini Burundi leo Machi 14, 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(MB)akitoa hotuba yake fupi kwa Maafisa na askari wa wa Jeshi la Magereza(hawapo pichani) kutoka vituo mbalimbali vya Magereza yaliyopo Mkoa wa Kagera alipotembelea Kambi ya Utenganisho ya Mwisa leo Machi 14, 2016.
Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakifuatilia kwa umakini mkubwa hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Hamad Masauni akitoa neno fupi kabla ya kumkaribisha rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kutoa hotuba yake fupi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, CGP John Casmir Minja akitoa taarifa fupi ya Hali ya Magereza nchini mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(hayupo pichani).
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiongea na Wakimbizi(walioketi chini) katika Kambi ya Mwisa inayosimamiwa na Jeshi la Magereza kwa kushirikiana na Shirika la kuwahudumia Wakimbizi Duniani(UNHCR). Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.