Monday, April 25, 2016

ARSENE WENGER ALILIA KUBAKI KWENYE 4 BORA

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema uwezekano wao wa kutofuzu kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI kwa mara ya kwanza katika Miaka 19 ni jambo la kutia wasiwasi.
Jumapili Arsenal walikosa nafasi ya kukamata Nafasi ya 3 kutoka ya 4 ya BPL, Ligi Kuu England baada ya kutoka 0-0 na Sunderland huko Stadium of Light.
Wenger ameeleza: "Tunajali na tuna wasiwasi kwa sababu sasa ni mapigano. Inakatisha tamaa kwani tulipigania Ubingwa na ukweli ni kuwa hatuwezi kuutwaa, inahuzunisha!"
Arsenal, ambao hawajamaliza nje ya 4 Bora tangu Msimu wa 1995/96, wapo Pointi 12 nyuma ya Vinara Leicester City huku Gemu 3 zimebaki.
Pia wako Pointi 5 mbele ya Timu ya 5 Man United ambao wana Mechi 1 mkononi na ni Timu 4 za juu ndizo zitacheza UEFA CHAMPIONS LIGI.
Akielezea kuhusu Mechi za mwisho wa Msimu, Wenger amedai zipo Klabu zenye Ratiba rahisi kwa kusema: "Kuna Ligi mbili wakati huu. Kuna Timu zimelegeza, zile ambazo ziko salama na haziendi Ulaya. Na unazo Timu za juu zinazogombea kitu na zilizo chini zinazopigana kutoshuka. Ni Gemu tofauti!"

MECHI ZILIZOBAKI:
Arsenal

-Norwich (H) Aprili 30
-Man City (A) Mei 8
-Aston Villa (H) Mei 15
Man United
-Leicester (H) Mei 1
-Norwich (A) Mei 7
-West Ham (A) Mei 10
-Bournemouth (H) Mei 15