Friday, April 1, 2016

ARSENE WENGER AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AJUZA SAFU YA MAJERUHI WAKE...

MENEJA wa Arsenal Arsene Wenger amesema Kiungo wake Jack Wilshere amerejea kwenye mazoezi kamili baada ya kupona Mguu wake uliovunjika.
Wilshere, mwenye Miaka 24 na ambae kwa Misimu Miwili sasa amekumbwa na majeruhi mfululizo, hajacheza kabisa Msimu huu baada ya kuumia katika Mechi za kujipima nguvu kabla Msimu kuanza hapo Agosti.
Awali ilikadiriwa kuwa Wilshere atakuwa nje kwa Mwezi Mmoja tu lakini baadae akalazimika kufanyiwa operesheni Mwezi Septemba.
Hata hivyo, kupona kwa Wilshere na kurejea mazoezini hakutamfanya aweze kucheza Mechi ya Wikiendi hii ya Arsenal dhidi ya Watford ya Ligi Kuu England.
Wenger pia alitoboa kuhusu hali za Majeruhi wake wengine ambapo Tomas Rosicky pia amerejea mazoezini pamoja na Kipa Petr Cech lakini Aaron Ramsey na Mathieu Flamini bado hawajawa fiti.
Wenger ameeleza: “Cech amerudi mazoezini lakini ni mapema mno kusema kama atacheza Wikiendi.”

Kipa Cech, ambae ndie Mchezaji pekee ambae Wenger alimsajili Msimu huu na kuwa nguzo thabiti, amekosa kuwepo Uwanjani kwa Wiki 4 tangu aumie hapo Machi 2 wakati Arsenal inachapwa 2-1 Uwanjani kwao Emirates na Swansea City.
Kuhusu, Santi Cazorla na Alex Oxlade-Chamberlain, hali zao bado hazijatengemaa ingawa Cazorla anaweza kurudi Uwanjani baada ya Wiki 3 au 4 kwani ameshaanza mazoezi ya kukimbia.

“We focus on giving our best until the end of the season, then we will judge the season.

“We have had many injuries as well. Let’s not judge too much. Our job is to perform until the last day of the season so let’s perform.”