Friday, April 29, 2016

BAYERN MUNICH JUMAMOSI KUFANYA MAAJABU TENA! WAKIWAFUNGA BORUSSIA MONCHENGLADBACH KUTWAA UBINGWA TENA!

Bayern Munich wapo njiani kuweka historia mpya huko Germany kwa kuwa Klabu ya kwanza kutwaa Ubingwa wa Bundesliga kwa mara ya 4 mfululizo ikiwa wataifunga Borussia Moenchengladbach ndani ya Allianz Arena Jijini Munich.
Bayern, chini ya Kocha Pep Guardiola, Juzi walifungwa 1-0 na Atletico Madrid kwenye Mechi ya Kwanza ya Nusu Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI huko Vicente Calderon Jijini Madrid, lakini Jumamosi wanaweza kusahau kipigo hicho na kushangilia.

Huku akilaumiwa kwa kuwapiga Benchi Mastaa wake Thomas Mueller na Franck Ribery kwenye Mechi na Atletico, Guardiola amekataa kusema ikiwa atawapumzisha Mastaa wengine kwenye Mechi hii na Borussia Moenchengladbach kwa sababu ya Marudiano yao na Atletico hapo Jumanne.
Hata hivyo, Mechi hii ya Jumamosi ni nafasi nzuri kwa Beki wao Jerome Boateng kurejea Uwanjani kwa mara ya kwanza tangu Januari alipoumia Nyonga.
Timu iliyo Nafasi ya Pili, Borussia Dortmund, ambayo iko Pointi 7 nyuma ya Bayern huku Mechi zikibaki 3, watakuwa kwao Signal Iduna Park kucheza VfL Wolfsburg.

BUNDESLIGA
RATIBA

Ijumaa Aprili 29
21:30 FC Augsburg v FC Koln

Jumamosi Aprili 30
1630 Bayern Munich v Borussia Monchengladbach
1630 BV Borussia Dortmund v VfL Wolfsburg
1630 Hannover 96 v Schalke 04
1630 FSV Mainz 05 v Hamburger SV
1630 TSG Hoffenheim v FC Ingolstadt 04
1630 Darmstadt v Eintracht Frankfurt
1930 Bayer 04 Leverkusen v Hertha Berlin

Jumatatu Mei 2 

21:15 SV Werder Bremen v VfB Stuttgart