Sunday, April 10, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: AZAM FC 2 v 1 ESPERANCE

BAO za Dakika ya 68 na 69 Leo zimewaponya Azam FC walipotoka nyuma kwa Bao 1-0 walipocheza na Esperance de Tunis ya Tunisia kwenye Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya CAF Kombe la Shirikisho iliyochezwa Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam.
Azam FC walitanguliwa kupigwa Bao katika Dakika ya 34 baada ya Haithem Jouini kuwatoboa lakini Bao 2 za ndani ya Dakika 1 zilizofungwa na Farid Mussa na Ramadhan Singano ziliwapa ushindi wa Bao 2-1 Azam FC.
Timu hizi zitaruadiana huko Tunis, Nchini Tunis na Mshindi kusonga Raundi ya Mchujo kusaka Timu 8 za kuingia Hatua ya Makundi na Azam wanahitaji Sare yeyote ile ili kusonga lakini wakifungwa 1-0 wako nje kwa Bao la Ugenini.