Wednesday, April 20, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO: ESPERANCE 3 vs 0 AZAM FC YANYUKWA NA KUTUPWA NJE!!

AZAM FC Jana huko Stade El Menzah, Mjini Tunis Nchini Tunisia ilipigwa Bao 3-0 na ES Tunis katika Mechi yao ya pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho na kutupwa nje ya Mashindano hayo.
Azam FC, ambao walishinda 2-1 katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Azam Complex, Chamazi Wiki 2 zilizopita, Jana walipigwa Bao zote 3 katika Kipindi cha Pili.
Bao hizo zilifungwa Dakika za 49, 64 na 81 na Saad Bguir, Haythem Jouini na Fakhreddine Ben Youssef.
Hivyo Azam FC wametupwa nje ya Mashindano haya na ES Tunis kusonga mbele kwa Jumla ya Mabao 4-2.