Wednesday, April 6, 2016

CHEIKHOU KOUYATE SASA HURU KUIKABILI ARSENAL JUMAMOSI HII

Kiungo wa kati wa West Ham Cheikhou Kouyate yuko huru kukabiliana na klabu ya Arsenal mechi ya Ligi ya Premia Jumamosi ijayo.
Hii ni baada ya Shirikisho la Soka la Uingereza kubatilisha kadi nyekundu aliyokuwa amepewa wakati wa mechi dhidi ya Crystal Palace Jumamosi.
Nyota huyo wa Senegal alifukuzwa uwanjani dakika ya 67 baada ya kumkaba Dwight Gayle, klabu yake ya West Ham ikiongoza 2-1 uwanjani Upton Park.
Mechi hiyo ilimalizika 2-2.
Kadi hiyo nyekundu ingemfanya Kouyate, 26, akose kucheza mechi hiyo ya nyumbani dhidi ya Gunners.

FA imesema kupitia taarifa: "Tume huru ya kusikiza malalamiko imeamua kwamba mchezaji huyo alifukuzwa uwanjani kimakosa.”