Monday, April 25, 2016

CHELSEA WANAOMBEA TOTTENHAM IKOSE UBINGWA UENDE LEICESTER CITY: EDEN HAZARD:

MCHEZAJI wa Chelsea Eden Hazard amesema yeye na Wachezaji wenzake wa Timu yake hawataki Tottenham watwae Ubingwa wa BPL, Ligi Kuu England.
Spurs wako Pointi 5 nyuma ya Leicester City huku Mechi zikiwa zimebaki 4 tu.
Chelsea ambao ndio walikuwa Mabingwa Watetezi wa BPL wataivaa Spurs Mei 2 Uwanjani Stamford Bridge na pia Leicester City hapo Mei 15 ambayo ndio Siku ya mwisho ya Msimu wa Ligi.

Akiongea na BBC, Shirika la Utangazaji la Uingereza, Hazard alisema: “Mashabiki, Klabu, Wachezaji, hatutaki Tottenham watwae Ubingwa Ligi Kuu!”
Aliongeza: "Tunaombea Leicester watwae kwa sababu wamestahili Msimu huu. Tuna Gemu nzuri Wiki ijayo dhidi ya Tottenham na kama tukiwafunga itakuwa vyema!”
Msimamo wa Hazard umeungwa mkono na Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas, ambae aliwahi kuwachezea Mahasimu wakubwa wa Tottenham wa London Kaskazini Arsenal kati ya 2003 na 2011, ambae pia anataka Leicester kutwaa Ubingwa kabla Chelsea hawajakutana na Tottenham.

Fabregas amesema: “Naamini Leicester watatwaa kabla ya hapo. Sitaki Spurs watwae Ubingwa lakini nadhani Leicester watautwaa na wanastahili!”