Monday, April 25, 2016

CLAUDIO RANIERI ASEMA SASA LAZIMA WASHINDE LIGI YA UINGEREZA

Mkufunzi wa kilabu ya Leicester Claudio Ranieri anaamini kwamba ni kazi ya kufa na kupona kwa klabu yake kushinda Ligi ya Uingereza.
Viongozi hao wa ligi wamekuwa na kampeni nzuri ya kushinda taji hilo na sasa wako pointi 8 juu ya klabu ya Tottenham ikiwa zimesalia mechi Tatu.
Kufikia sasa klabu hiyo ina hakika ya kushiriki katika mechi za klabu bingwa Ulaya baada ya kujihakikishia kumaliza katika timu tatu bora, na Ranieri anasema kuwa lengo lake kuu sasa ni kushinda taji la ligi.''Ni mwaka huu ama isifanyike tena''.

''Tumefanikiwa kufuzu katika michuano ya kombe la vilabu bingwa,ni ufanisi mkubwa kwa kila mtu lakini sasa tunajaribu kushinda taji la ligi na nguvu zetu zote.

Nimewaambia wachezaji wangu kwamba sasa ndio wakati mzuri wa kuweka nguvu zote.Tunahitaji pointi tano tushinde taji. Na tutajaribu kufanya hivyo