Friday, April 8, 2016

CLAUDIO RANIERI NA HARRY KANE NDIYO BORA, WATWAA TUZO MWEZI MACHI

CLAUDIO RANIERI na Harry Kane wametwaa Tuzo za Ligi Kuu England, BPL, Barclays Premier League, kwa Meneja na Mchezaji Bora kwa Mwezi Machi.
Hii ni mara ya pili kwa Ranieri, Meneja wa Leicester City kutoka Italy mwenye Miaka 64, kutwaa Tuzo hii akiiongoza Timu yake kukaa kileleni mwa BPL ikielekea kutwaa Ubingwa.
Leicester wanaongoza BPL wakiwa Pointi 7 mbele ya Tottenham Hotspur.

Mwezi Machi uliwapa Leicester ushindi wa Mechi 3 bila kufungwa Bao kwa kuzifunga Watford, Newcastle na Crystal Palace 1-0 kila Mechi na kujichimbia kileleni.
Nae Harry Kane, Straika wa Tottenham mwenye Miaka 22, amekuwa moto kwa kupiga Bao 5 katika Mechi 4 za Mwezi Machi.