Friday, April 15, 2016

DROO NUSU FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE: RONALDO KUREJEA JIJINI MANCHESTER, MAN CITY vs REAL MADRID, ATLETICO MADRID vs BAYERN MUNICH

Manchester City watakutana na Real Madrid kwenye Nusu Fainali ya UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI baada ya kufanyika Droo ya kupanga Mechi hizo hii Leo huko Nyon, Uswisi.

Nusu Fainali nyingine ni kati ya Bayern Munich na Atletico Madrid.
Mechi za Kwanza za Nusu Fainali zitachezwa Aprili 26 na 27 na Marudiano ni Mei 3 na 4 huku Fainali ikichezwa huko Mjini Milan, Nchini Italy kwenye Uwanja wa San Siro hapo Mei 28.

Droo hii ya Leo inamaanisha Straika wa Real Cristiano Ronaldo, ambae ndie Mfungaji Bora wa Mashindano haya akiwa na Bao 16, anarejea Jijini Manchester ambako aliwahi kuchezea Mahasimu wa Man City, Manchester United.

Ronaldo, mwenye Miaka 31, pia ndie anaongoza katika Ufungaji Bora wa Mashindano haya katika Historia akiwa na Bao 93 katika Mechi 125.