Thursday, April 14, 2016

DROO UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUFANYIKA LEO IJUMAA....MAN CITY, BAYERN, ATLETICO, REAL MADRID KUJUA WAPINZANI NUSU FAINALI

KLABU 4 za Ulaya zinasubiri Droo ya kupanga Mechi za Nusu Fainali za UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI, ambayo itafanyika Ijumaa Aprili 15 huko Nyon, Uswisi kuanzia Saa 6 na Nusu Mchana.
Klabu ambazo zitakuwemo kwenye Chungu cha Droo hiyo ni Klabu 2 Mahasimu wa Spain, Real Madrid na Atletico Madrid, Bayern Munich ya Germany na Manchester City ya England ambao ni mara ya kwanza kabisa kutinga hatua hii.

Droo hii, ambayo ni huru, inamaanisha inaweza kuleta uhondo wa Mechi kati ya Mahasimu wa Jiji la Madrid, Real na Atletico, na ile Mechi kati ya Man City na Bayern huku mvuto ukiwa Meneja wa Bayern, Pep Guardiola, ambae tayari ni rasmi kuwa mwishoni mwa Msimu huu atamalizana na Bayern na kwenda Man City.