Sunday, April 24, 2016

FA CUP FAINALI SASA NI MANCHESTER UNITED v CRYSTAL PALACE, WEMBLEY MEI 21.

Crystal Palace leo wametinga Fainali ya FA CUP baada ya kuifunga Watford United Bao 2-1 kwenye Nusu Fainali iliyochezwa Uwanjani Wembley, Jijini London.
Kwenye Fainali, itakayochezwa hapo hapo Wembley hapo Mei 21, Palace watakutana na Manchester United ambao Jana waliwatoa Everton 2-1 katika Nusu Fainali nyingine.
Hadi Mapumziko Palace walikuwa mbele kwa Bao 1-0 lililofungwa na Yannick Bolasie. 


Kipindi cha Pili, Watford walimudu kusawazisha kupitia Deeney lakini Dakika 6 tu baadae Connor Wickham akafunga Bao la Pili na la ushindi kwa Palace.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Crystal Palace kufika Fainali ya FA CUP na mara ya kwanza ni Mwaka 1990 walipofungwa na Man United.