Thursday, April 21, 2016

FA CUP: NUSU FAINALI NI WIKIENDI HII WEMBLEY, MAN UNITED vs EVERTON, PALACE vs WATFORD

WIKIENDI hii huko England zipo Mechi za BPL, Ligi Kuu England lakini pia zipo Mechi za Nusu Fainali za Kombe kongwe kabisa Duniani, FA CUP, ambalo kwa sababu za kiudhamini linaitwa EMIRATES FA CUP.
Jumamosi ni Nusu Fainali ya kwanza kati ya Manchester United na Everton na Jumapili itachezwa Nusu Fainali ya Pili kati ya Crystal Palace na Watford United.

DONDOO:
-Mechi za Nusu Fainali inazikutanisha Timu za Ligi Kuu England pekee.
-Mechi zote zitachezwa Uwanja wa Wembley Jijini London Jumamosi Aprili 23 na Jumapili Aprili 24.
-Fainali ya FA CUP itachezwa pia Uwanjani Wembely hapo Mei 21.

FA CUP – Historia ya Timu hizi 5:
Crystal Palace – Wamefika Fainali mara 1 tu Mwaka 1990 na kufungwa na Man United.

Everton – Wametwaa Kombe hili mara 5 lakini mara ya mwisho ni Mwaka 1995 (Wamelibeba Miaka ya: 1906, 1933, 1966, 1984, 1995). Pia wamefika Fainali mara 8 na ya mwisho ilikuwa 2009 chini ya David Moyes walipofungwa na Chelsea.

Watford – Wamefika Fainali mara 1 tu Mwaka 1984.

West Ham United - Wametwaa Kombe hili mara 3 lakini mara ya mwisho ni Mwaka 1980. (Wamelibeba Miaka ya: 1964, 1975, 1980). Pia wametinga Fainali mbili ikiwemo ile ya 2006 waliyofungwa na Liverpool.

Manchester United – Kati ya Timu hizi 5, Man United ndio wababe kwa kubeba FA Cup mara 11 lakini mara ya mwisho ni 2004.