Thursday, April 7, 2016

FIFA LISTI YA BORA DUNIANI: ARGENTINA NAMBA 1, TANZANIA YAPOROMOKA CHINI NAFASI 5 NI YA 130

FIFA Leo imetoa Listi mpya ya Ubora Duniani na Argentina wamekamata Namba 1 kwa kuishusha Belgium iliyokamata Namba 2.
Tanzania imeporomoka Nafasi 5 na sasa ipo ya 130.
Kwa Afrika, Nchi ya juu ni Algeria ambayo iko Nafasi ya 33 baada ya Cape Verde kuporomoka Nafasi 16 na kukamata Nafasi ya 47.
Inayofuatia kwa Arika ni Ivory Coast iliyo Nafasi ya 34.
Mabingwa wa Dunia Germany wapo Nafasi ya 5.
Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa Mei 5.
10 BORA:
1 ARGENTINA
2 BELGIUM
3 CHILE
4 COLOMBIA
5 GERMANY
6 SPAIN
7 BRAZIL
8 PORTUGAL
9 URUGUAY
10 ENGLAND